Morrison ashinda tuzo Simba

351

Kiungo mshambuliaji, Bernard Morrison amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Novemba (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Morrison raia wa Ghana amewashinda mshambuliaji Medie Kagere na kiungo Jonas Mkude ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Katika mwezi Novemba, Morrison amecheza jumla ya dakika ya 235 akifunga mabao mawili na kusaidia kupatikana kwa mengine mawili.

Baada ya kushinda, Morrison amekabidhiwa kitita cha Sh 2,000,000 kama sehemu ya zawadi kutoka kwa wadhamini wa tuzo hizo Kampuni ya Emirate Aluminium ACP.

Tuzo hiyo mwezi Octoba ilichukuliwa na Hassan Dilunga.

Mchanganuo wa kura ulivyokuwa;

Bernard Morrison kura 2117 (46.77%)
Meddie Kagere kura 2115 (46.73%)
Jonas Mkude kura 294 (6.50%)

Author: Asifiwe Mbembela