Niyonzima aongeza kandarasi Yanga, sasa kuendelea kukipiga Jangwani

283
Licha ya kutopata nafasi ya kucheza kama ilivyokuwa imezoeleka, kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda Haruna Hakizimana Niyonzima ‘Fabregas’ amejifunga pingu na mabingwa wa kihistoria wa VPL Yanga SC.
Niyonzima alitua Timu ya Wananchi kwa awamu ya pili baada ya misimu miwili kukitumikia kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba ‘dhimba’.
Kupitia ukurasa rasmi wa mmoja wa viongozi wa juu wa GSM lakini pia mshauri katika masuala ya usajili Hersi Said ameweka picha na kueleza kifupi kama kiungo huyo mwenye uchezaji wa aina yake sawa sawa na mikogo yake.
Haruna Niyonzima alianza kupoteza nafasi chini ya kocha Zlatico Krmpotick ambapo licha ya kukosa nafasi ya kucheza bado Zlatico alikuwa anampa nafasi kuliko ilivyo chini ya Cendric Kaze ambaye amekuwa mara nyingi akimpa angalau dakika 10 za mwisho katika mechi za mashindano.
Niyonzima alijiunga na Yanga miaka tisa iliyopita ambapo alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichobeba taji la VPL mara tatu.

Author: Asifiwe Mbembela