Simba Watua Morocco, Yawafuata Raja Casablanca

226

Kundi la kwanza la kikosi cha Simba wamefanikiwa kufika salama Rabat, Morocco kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa mwisho hatua ya makundi na Raja Casablanca utakaochezwa mwishoni mwa wiki hii.

Wachezaji ambao wameondoka kwenda huko ni wale ambao hawakuwa sehemu ya timu zao za taifa pamoja na wale ambao wamewai kurudi kutoka kwenye kamba za timu zao za taifa.

Pamoja na safari hiyo kupata mshikeli kidogo na kulazimika kutua Arusha kwa dharura, kikosi hicho kimetua Morocco ukiwa ni mchezo wa kukamilisha ratiba kwani timu hizo mbili zimeshafuzu kwenda hatua ya robo fainali.

Baadhi ya wachezaji waliosafiri ni Joash Onyango, Israel Mwenda, Kennedy Juma, Kiyombo na Gadiel Michael.

Author: Asifiwe Mbembela