Taddeo Lwanga ajumuishwa kwenye kikosi cha Simba kuelekea Zimbabwe kuwakabili FC Platinum

535

Kikosi cha Simba Disemba 18 kimekwea pipa kuelekea nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.

Wakati kikosi hicho kikianza safari baadhi ya majina ya mastaa wa kikosi hawajaonekana kwenye listi ya wanadinga watakaotua pale Harare.

Wachezaji hao ni pamoja na Charles Ilanfya ambaye ni mshambuliaji namba nne wa Simba, na Bernard Morrison ambaye sababu za kuwa nje bado hazijafahamika.

Hata hivyo ingizo jipya la Taddeo Lwanga yuko katika sehemu ya kikosi ambacho kimesafiri kuwafuata Platinum.

Simba itacheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa Desemba 23 na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Januari 6, Uwanja wa Mkapa.

Ikiwa itashinda kwenye mchezo wa kwanza na kuweza kulinda ushindi wake kwenye mchezo wa marudio utakaochezwa Bongo, Simba inaweza kutinga hatua ya makundi.

Kikosi kilichosafiri ni:-

Golikipa: Aishi Manula, Ally Salim na Beno Kakolanya,

Walinzi: Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Josh Onyango, Ame Ibrahim.

Viungo: Clatous Chota Chama, Hassan Dilunga, Jonas Mkude, Hamis Ndemla, Larry Bwalya, Mzamiru Yasni, Luis Miqussone, Miraji Athumani, Taddeo Lwanga, Fransis Kahata, na Ibrahim Ajibu.

Washambuliaji: Meddie Kagere, John Raphael Bocco, na Chris Mugalu,

Author: Asifiwe Mbembela