Tetesi za Mastaa Ulaya: Babake Messi aendeleza mazungumzo na Barcelona, Suárez akimbilia Juventus

271

Rais wa Napoli Aurelio de Laurentiis amesema anahitaji kumsajili beki wa kati wa Arsenal na Ugiriki mwenye umri wa miaka 32 Sokratis Papastathopoulos, jambo linaloashiria kuwa mlinzi wa timu hiyo na Senegal Kalidou Koulibaly, 29, ataondoka na kujiunga na Manchester City. De Laurentiis amesema alikataa kumuuza mapema staa wake Koulibaly 29, kwenda kwenye timu ambazo zinamhitaji ili kutengeneza pesa ndefu zaidi.

Babake Lionel Messi ametumia siku ya pili kujadiliana na klabu ya Barcelona juu ya hatima ya mtoto wake ambaye anahusishwa kusajiliwa na mabwenyenye wa Manchester City ya nchini England.

Strika wa Barcelona na Uruguayi Luis Suárez yuko mbioni kujiunga na miamba ya soka la Italia Juventus na kukutana na mchezaji mweza Giorgio Chiellini.

Beki wa kati wa Manchester United Chris Smalling, 30, ambaye alikuwa kwa mkopo katika klabu ya Roma anakaribia kujiunga na timu hiyo kwa mkataba wa kudumu.

Manchester United wanajaribu kujaribu bahati yao ya kumsajili winga wa Borrusia Dortmund Jadon Sancho 20 ingawa changamoto kubwa ni kutofautiana kwa dau la usajili na masuala binafsi ya mchezaji huyo.

Author: Bruce Amani