Tetesi za Mastaa Ulaya: Arthur wa Barcelona mbioni kujiunga na Juventus

333

Kiungo mshambuliaji wa Barcelona na Brazil Arthur, 23, yuko mbioni kujiunga na miamba ya soka la Italia Juventus kwa dau linalokadiriwa kufikia pauni milioni 73 wakati huo huo kiungo mkabaji wa Bosnia-Herzegovina Miralem Pjanic, 30 akielekea Barca kwa dau la pauni milioni 54.3.

Winga wa Chelsea Pedro, 32, atajiunga na Roma kwa mkataba wa miaka miwili baada ya mkataba na Chelsea kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Bayern Munich wamekataa kujiunga kwenye mbio za kumuwania staa ambaye Manchester United pia wanamwinda Jude Bellingham, 16, licha ya tetesi kusema wamemalizana na Borrusia Dortmund.

Arsenal walikuwa tayari kumlipa winga wa Chelsea Willian, 31, mshahara wa £250, 000 kabla ya kuibuka kwa virusi vya Corona.

Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amemwambia Mwenyekiti wa klabu Daniel Levy kuwa anahitaji saini ya wachezaji watano, lakini Spurs imesema ipo tayari kuwapata wachezaji huru na wachezaji wa mikopo.

Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers amemwambia kiungo wake James Maddison, 23, kuwa kubakia klabuni hapo ni jambo la heri kuliko kwenda kwingineko kama Manchester United.

Author: Bruce Amani