Viingilio, Waamuzi Simba, Yanga bayana

368

Wakati presha ya mchezo ikiendelea kupanda kwa Watani wa Jadi baina ya wenyeji Simba na Yanga utakaopigwa dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Disemba 11, Shirikisho la Kandanda nchini Tanzania TFF limetoa majina ya Waamuzi ambao watachezesha pamoja na viingilio vya mchezo huo.

Simba Sc itakuwa na kibarua hicho baada ya kutoka kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika na kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Kombe hilo ikiwa ni mara ya kwanza wakati Yanga mechi ya mwisho ilikuwa dhidi ya Mbeya Kwanza ambayo walishinda 2-0.

Shirikisho na klabu ya Simba ambao ni wenyeji wa mtanange huo wametangaza viingilio vya mchezo huo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Kiingilio cha chini katika mchezo huo wa Desemba 11 kitakua Shilingi 5,000 huku kiingilio cha juu kimetajwa kuwa Shilingi 30,000.

Tayari Mabingwa wa Ligi wa kihistoria Yanga wameshaanza maandalizi ya mchezo huo, huku Simba SC ikitarajia kuanza kambi mara itakaporejea Dar es salaam, ikitokea Lusaka-Zambia ilipokua inakabiliwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho mkondo wa pili hatua ya mtoano dhidi ya Red Arrows.

Mchezo huo uliochezwa Jumapili (Desemba 05), Simba SC ilipoteza kwa kufungwa 2-1, lakini imefuzu hatua ya Makundi kwa ushindi wa jumla wa 4-2.

Pia waamuzi wametajwa ambapo mwamuzi wa kati atakuwa Herry Sasi, akisaidiwa na Kassim Mpanga, na Hamdani Saidi.

Author: Asifiwe Mbembela