Wadau Wahamasishwa Zaidi Kununua Tiketi Kuitazama Taifa Stars

98

Wadau wa kabumbu nchini wameendelea kununua tiketi kwa ajili ya mashabiki watakaoingia kuutazama mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON 2023 nchini Ivory Coast dhidi ya Uganda.

Tiketi ambazo zinanunuliwa zinawapa nafasi mashabiki kwenda kwa wingi kuutazama mchezo huo utakaochezwa Machi 28 na kwa kutoa hamasa kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Stars inahitaji alama tatu kwenye mchezo na Uganda ili kufikisha pointi 7 ambazo zitawaweka kwenye eneo nzuri kuwania nafasi ya kushiriki AFCON ijayo kwa mara tatu katika historia ya taifa la Tanzania.

Baadhi ya wadau ambao wamenunua tiketi ukiachia tiketi 2,000 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, wengine ni Rais wa Yanga, Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Simba, taasisi ya kifedha ya CRDB pamoja na wadau wengine.

Shirikisho la soka nchini TFF limeendelea kuhamasisha wadau kujitokeza zaidi kununua tiketi kwa ajili ya mashabiki.

Author: Asifiwe Mbembela