Bayern ndio mabingwa wa DFB Pokal baada ya kuwabwaga Bayer Leverkusen

336

Bayern Munich imefanikiwa kuibuka kidedea kwa goli 4-2 dhidi ya Bayer Leverkusen katika fainali ya Kombe la Ligi ya Ujerumani uliopigwa dimba tupu la Olympic Jana Jumamosi.

Wakati Bayern wakibeba taji hilo straika hatari wa timu hiyo Roberto Lewandowski ameandikisha rekodi ya aina yake baada ya kufunga goli 2 kwenye ushindi huo, mabao yanayomfanya kufikisha goli 51 katika jumla ya michezo 44 aliyocheza msimu huu.

Faulo ya David Alaba katika dakika za mapema iliwapa uongozi Bayern Munich kabla ya straika wa zamani wa Arsenal Serge Gnabry kufunga goli la pili na baada ya hapo Lewandowski akafunga goli lake la kwanza.

Goli la kichwa la Sven Bender liliwapa matumaini Leverkusen ingawa msumari wa Lewandowski uliwarudishia machungu katika mtanange huo.

Keki katika usajili barani Ulaya msimu huu, Kai Havertz alifunga goli kwa njia ya tuta lakini halikutosha kufuta kipigo dhidi ya Bayern Munich ambayo walikuwa bora katika idara zote.

Ushindi huo unaifanya Bayern Munich kuandikisha rekodi ya kucheza mechi 26 bila kupoteza hata mchezo mmoja, sare moja tu kati ya hizo tangu mwezi Disemba.

Baada ya kushinda Bayern watakuwa wanatazamia kutwaa mataji matatu msimu huu (treble) endapo watashinda taji la Uefa kwani hatua ya 16 bora ni kama wameshafuzu baada ya kuichapa Chelsea goli 3-0 raundi ya kwanza ya hatua hiyo.

Wakati huo huo, Leverkusen wanaongoza kwa goli 3-1 dhidi ya Rangers katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya 16 bora wa ligi ya Europa.

Author: Bruce Amani