Lyon wagoma kumuachia Houssem Aouar kwa Arsenal, Tottenham yamwinda Lingard

166

Tottenham wanataka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Manchester United na England Jesse Lingard, 27, kwa ada ya pauni milioni 30.

Wagonga Nyundo wa London West Ham United wamewaambia Chelsea kuwa kiungo wao mkabaji Declan Rice, 21, sio wa kuuzwa kwa bei yoyote ile.

Manchester City wametuma ofa ya pauni milioni 50.4 kwa mlinzi wa Kifaransa Jules Kounde, 21, licha ya kwamba dau hilo kupigwa chini na Sevilla.

Chelsea wameafikiana na klabu ya Rennes juu ya kumleta kipa raia wa Senegal Edouard Mendy 28, ada ya pauni milioni 22 kutumika kwenye uhamisho huo.

Barcelona wamezuiliwa kumsajili kiungo mkabaji wa Liverpool Georginio Wijnaldum kutokana na kanuni za La Liga za kiuchumi.

Wolves wanavutiwa kumsajili winga wa zamani wa Arsenal na sasa Liverpool Alex Oxlade-Chamberlain, 27.

Leeds United watajaribu kumsaini winga wa Manchester United na Wales Daniel James, 22, endapo tu atashindwa kupata nafasi kikosi cha kwanza.

Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amesema Arsenal hawatafikia dau la kiungo wao ambaye ni raia wa Ufaransa Houssem Aouar, 22.

Kwa mjibu wa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Colombia Banfield amesema kiungo mchezeshaji James Rodriguez amejiunga na Everton huru bila pesa yoyote akitokea Real Madrid.

Author: Bruce Amani