Bayern watinga fainali kwa kuwatandika Al Ahly 2-0 Kombe la Dunia ngazi ya vilabu 2021

379

Bayern Munich wametinga hatua ya fainali ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu baada ya kuwaadhibu klabu ya Misri Al Ahly kwa goli 2-0 katika mchezo uliopigwa Leo Jumatatu mjini Doha Qatar.

Magoli ya Bayern yamefungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Poland Robert Lewandowski kunako dakika ya 17 na 86 akimalizia krosi maridhawa ya Leroy Sane aliyeingia kutokea benchi.

Inakuwa mara ya tatu mfululizo Al Ahly ambayo inaliwakilishi bara la Afrika kupoteza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia ngazi ya vilabu katika misimu mitatu tofauti.

Bayern Munich wataingia mchezo wa fainali kutafuta taji la kwanza la msimu dhidi ya Tigres ya Mexico ambayo iliifunga Palmeiras ya Brazil 1 – 0.

Author: Bruce Amani