Messi aiongoza Barcelona kushinda 3-2 kwa Real Betis

116

Staa wa Barcelona na Argentina Lionel Messi alitumia dakika tatu pekee kufunga goli baada ya kutokea benchi na kukiongoza kikosi cha timu hiyo kushinda 3-2 mbele ya Real Batis.

Wenyeji Betis walitumia vyema faida ya kuwa nyumbani na kutangulia kupata goli la mapema kupitia kwa Borja Iglesias, lakini Messi aliyekuwa amepumzishwa na kocha Ronald Koeman aliingia dakika ya 57 na kusawazisha kabla ya Victor Ruiz kujifunga na kuwapa uongozi Barca.

Baada ya kujifunga Ruiz alifunga goli lingine kwa upande wa timu yake kabla ya Trincao kufunga goli pekee.

Barcelona wamekwea mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga mbele yao kuna Atletico Madrid wakiwa nyuma kwa alama saba licha ya wao kuwa na mchezo mmoja mkononi.

Author: Bruce Amani