Man City yaitandika Swidon, Kombe la FA

126

Manchester City imeshinda bao 4-1 mechi yake na timu ya daraja pili Swindon katika mchezo wa Kombe la FA hatua ya tatu huku timu hiyo ikiwa chini ya kocha msaidizi Rodolfo Borrell baada ya Pep Guardiola kubainika kuwa na viashiria vya Covid-19.

Bao za Manchester City zimetumbukizwa kimiani na kiungo mshambuliaji wa Ureno Bernando Silva akimalizia pasi ya kinda Cole Palmer, Gabriel Jesus, Ilkay Gundogan kabla ya kinda Palmer kufunga goli lake la kwanza kwenye mashindano ya FA.

Harry McKirdy alifunga goli la kufuatia machozi kwa upande wa timu ya Swindon na kufanya matokeo kuwa 4-1 katika dakika 90 za mchezo huo.

Author: Bruce Amani