Man United yakatisha rekodi bab kubwa ya watani wao Man City kwa kuwachapa 2-0

122

Manchester United imeivunjilia mbali rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Manchester City ya kushinda mechi 21 mfululizo katika mashindano yote baada ya kuifunga bao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England uliopigwa dimba la Etihad Leo Jumapili.

Pep Guardiola na kikosi chake licha ya kupoteza bado wanaonekana wanaenda kutwaa ubingwa wa EPL hasa baada ya pengo la alama kuwa 11, huku ushindi muhimu kwa Ole Gunnar Solskjaer ukiifanya United kurejea nafasi ya pili.

United ambao wamefikisha mechi 22 ugenini bila kupoteza ukijumulisha na mechi 14 za ushindi walitangulia kujipatia bao kupitia kwa kiungo mshambuliaji raia wa Ureno Bruno Fernandes akifunga kwa njia ya penati baada ya strika Gabriel Jesus kumfanyia faulo mshambuliaji Anthony Martial sekunde ya 30.

Dakika 45 za kwanza zilimalizika kwa United kuwa kiongozi lakini beki wa kushoto wa Manchester Luke Shaw aliongeza bao la pili akitumia vyema pasi ya winga matata Marcus Rashford baada ya shambulio la hatari.

Solskjaer alikuwa hajafunga goli katika mechi tatu zilizopita amerudi nafasi ya pili alama moja dhidi ya Leicester City ambao Jana walishinda 2-1 kwa Brighton.

Author: Asifiwe Mbembela