MO aanzisha kuchangia kujenga Uwanja Simba

523

Baada ya tukio la Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Barbara Gonzalez kuzuiliwa kuingia uwanjani katika mchezo wa Watani wa Jadi baina ya Simba wenyeji na Yanga kwa kile kichoelezwa kuwa alikiuka utaratibu wa TFF na TPLB, Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara wameamua kuanzisha mpango wa kujenga uwanja wao ikiwa ni sehemu ya kukwepa matukio kama hayo.

Katika kuhanikiza hilo, Mwekezaji ndani ya Wekundu wa Msimbazi Simba, Mohamed ‘Mo’ Dewji ameahidi kutoa Sh. Bilioni 2 ili wanachama wajazie klabu hiyo ijenge Uwanja wake kwa mechi zake za mashindano ya ndani na ya Kimataifa.

“Nimepokea maoni mengi ya WanaSimba wenzangu wakishauri tujenge uwanja wetu na wako tayari kuchangia ili tufanikishe ujenzi huo,” ameandika Dewji katika ukurasa wake.
“Naomba kuweka wazi kwamba nimepokea maoni hayo kwa mikono miwili. Naomba Bodi ya Simba kukaa na kuja na utaratibu wa haraka ili jambo hili lianze utekelezaji,”.

“Kwa kuanza naahidi kuchangia Tsh. 2 bilioni. Nawaomba wanasimba tuchangie sote,”.

Kwa sasa Simba ina Uwanja wa mazoezi tu, Mo Simba Arena uliopo Bunju Jijini Dar es Salaam, ambapo mechi zote za mashindano rasmi inatumia uwanja wa Benjamin Mkapa.

Author: Asifiwe Mbembela