Real Madrid yavuna ushindi kwa Atletico Madrid

453

Real Madrid imeibuka na ushindi wa goli 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga dhidi ya Atletico Madrid ukiwa ni ushindi wa 10 mfululizo kwa klabu hiyo.

Madrid wanafikisha tofauti ya alama nane kwa timu iliyo nafasi ya pili Sevilla ambapo sasa kwa zile timu tarajiwa kwenye ubingwa Barcelona na Atletico kuwa mbali nao.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Karim Benzema alifunga goli la kwanza kwa shuti kali akimalizia kazi nzuri ya Vinicius Junior ambaye msimu huu yuko kwenye ubora mkubwa.

Bao la pili likiwekwa kimiani na Marco Asensio kazi ya Vinicius Junior tena ambaye mbali na kutofunga lakini unaweza kumtaja kama mchezaji bora wa mechi.

Inaonekana kocha Carlo Ancelotti amekiwezea kikosi hicho kwani mara ya mwisho kupoteza mechi ilikuwa Octoba 3, katika mechi 23 wamepoteza mechi mbili.

Author: Bruce Amani