Real Madrid yaibutua Sevilla na kukamata usukani

Real Madrid imekwea alama tatu zaidi ya mabingwa watetezi wa La Liga Barcelona baada ya ushindi dhidi ya Sevilla mtanange uliopigwa dimba la Bernabeu leo Jumamosi.

Kiungo wa Kibrazil Casemiro ameibuka kinara katika kufumania nyavu za Sevilla katika mchezo huo kwa kufunga goli mbili kabla ya goli la kufutia machozi la Luuk de Jong.

Licha ya Real Madrid kuongoza, Barcelona wanaweza wakarudi kileleni mwa msimamo wa La Liga endapo tu wataibuka na ushindi dhidi ya Granada siku ya Jumapili.

Matokeo hayo kwa wageni Sevilla yanamaanisha kuwa itaendelea kusalia nafasi ya nne huku kikosi cha kocha wa zamani wa Madrid Julen Lopetegui walikuwa wanategemewa kuendeleza hofu kwa vinara wa ligi hiyo endapo ingeshinda.

Author: Bruce Amani