Ronaldo Aweka Rekodi Kibao Duniani, Atupia Mbili Mbele ya Liechtenstein

178

Cristiano Ronaldo amefikisha mechi 197 ngazi ya timu ya taifa na kuwa mchezaji wa kwanza kufikia rekodi hiyo kwani awali ilikuwa inashikiliwa na Bader Al-Mutawa wa Kuwait ambaye alikuwa amecheza mechi 196.

Hata hivyo, Ronaldo kucheza leo kumemfanya kuwa mchezaji wa kwanza, katika mtanange huo ameweza kufunga magoli mawili kwenye ushindi wa bao 4-0 walioupata Ureno dhidi ya Liechtenstein katika kuwania kufuzu michuano ya Euro 2024.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 38, magoli ambayo ameyafunga yanaendelea kuimarisha historia yake ambapo sasa amefikisha bao 120 za kimataifa.

Baada ya kuanza taaluma yake mwaka 2003, staa wa zamani wa Manchester United, Real Madrid, Juventus na Nassr katika fainali za Kombe la Dunia Qatar aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga angalau bao kwenye mechi za WC.

Author: Bruce Amani