Simba Kuitangaza Tanzania Kimataifa

713

Kuelekea mtanange wa Kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya makundi mchezo wa kwanza baina ya wenyeji Simba Sports Club na ASEC Mimosas, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amemkabidhi Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez jezi yenye ujumbe wa kuitangaza nchi.

Jezi ambazo Simba wamekabidhiwa Leo Ijumaa Februari 11, 2022 ni zile ambazo zitavaliwa kwenye mashindano yote ya msimu huu kumbuka hata msimu uliopita kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Simba ilitumia jezi zenye nembo hizo.

Kwa nini isitumie jezi zenye nembo ya mdhamini wa kwenye Ligi, Shirikisho la Kandanda Afrika mdhamini mkuu wa mashindano yake anajihusisha na shughuli ambazo mdhamini wa Ligi anafanya.

Zoezi la kukabidhiwa jezi limefanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.

Simba watatumia jezi hizo kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kuanzia Jumapili kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa Kundi D dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast Saa 10:00 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Author: Asifiwe Mbembela