Tanzania yakabwa shati na Rwanda mjini Kigali

285
Timu ya Taifa ya Tanzania imetoa suluhu ya bila kufungana na taifa la Rwanda ‘Amavubi’ katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa nchini Rwanda leo Jumatatu ukiwa katika kalenda ya FIFA.
Tanzania ambayo ipo chini ya Kaimu kocha mkuu Ettiene Ndayairagije ameshindwa kufunga magoli katika michezo ya hivi karibuni huku wakishindwa kutulia katika eneo la ushambuliaji.
Katika mchezo wa leo dimba la kati likitumika kwa kiasi kikubwa na timu zote huku mtanange ukiwa na ushindani mkubwa kwa dakika zote tisini.
Kocha msaidizi wa Taifa Stars, Seleman Matola amesema kuwa wachezaji walipambana kupata matokeo ila bahati haikuwa yao.
Baada ya mchezo leo, Tanzania itaunganisha safari ya maandalizi ya kujiandaa na mchezo wa kiushindani dhidi ya Sudan ambapo mtanange wa awali uliopigwa Dar es Salaam Taifa Stars ilifungwa goli 1-0 huku Tanzania wakihitaji kushinda zaidi ya goli 2 ili kufuzu makundi ya Chan- Michuano ya Wachezaji wa ndani

Author: Bruce Amani