Tetesi za Mastaa Ulaya: Alaba kuramba dili Real Madrid, Liverpool yamnyemelea Dembele wa Barca

247

Chelsea wanavutiwa kumsajili kiungo mkabaji wa Borrusia Dortmund na England Jude Bellingham, 17, kwa mjibu wa klabu yake inasema Jude anapatikana kwa dau la pauni milioni 100.

Manchester United wameanza mapema kufanya mazungumzo na mlinzi kijana wa Leicester City Wesley Fofana, 20.

Liverpool wanahitaji kupata saini ya winga wa Kifaransa na Barcelona Ousmane Dembele, 23, kama mbadala wa Sadio Mane, 29.

Mlinzi wa kati wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 28, kuna uwezekano mkubwa akajiunga na miamba ya soka ya Real Madrid baada ya kutangaza kuwa hataendelea na timu mwishoni mwa msimu huu.

Author: Bruce Amani