Nyota 28 Simba tayari kupambana na Mwadui, Kagera Sugar na Gwambina Kanda ya Ziwa

172

Nyota 28 wa kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya Simba kimeondoka kuelekea Mikoa ya Nyanda ya Ziwa kwa ajili ya michezo mitatu ya Ligi ukiwa mtanange dhidi ya Mwadui utakaopigwa kesho Jumapili.

Simba ambayo ilikuwa kwenye majukumu ya kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, ilirejea wiki iliyopita na kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar na kushinda bao 5-0.

Kwa mujibu wa tovuti ya Simba imeandika kuwa Kocha Didier Gomez na wasaidizi wake, wameamua kuondoka na kikosi kizima kutokana ugumu wa mechi huku timu zote zikiwa zimejipanga kipindi hiki cha lala salama ligi ikielekea ukingoni.

Ratiba ya michezo hiyo Kanda ya Ziwa itaanza Jumapili ambapo itashuka kwenye Uwanja wa Kambarage Shinyanga kuikabili Mwadui na siku tatu baadaye (Jumatano) itacheza na Kagera Sugar Kaitaba kabla ya kumalizana na Gwambina Aprili 24.

Kikosi Kamili kitakachokwenda Kanda ya Ziwa;

Makipa:- Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim

Mabeki:-Shomari Kapombe, Joash Onyango, Pascal Wawa, Ibrahim Ame, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Mohamed Hussein, Kennedy Juma, David Kameta

Viungo:Jonas Mkude, Rally Bwalya, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Luis Miquissone, Hassan Dilunga, Clatous Chama, Bernard Morrsion, Francis Kahata, Taddeo Lwanga.

Washambuliaji:Medie Kagere, John Bocco, Ibrahim Ajib, Kope Mugalu, Miraji Athumani, Perfect Chikwende.

Author: Asifiwe Mbembela