Tetesi za Mastaa Ulaya: Arsenal Yajitosa kwa Rashford wa Man United

146

Arsenal wanajiandaa kutupa karata yao kuona namna ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa England na Manchester United Marcus Rashford, 24.

Uongozi wa EPL umeizuia klabu ya Burnley kumsajili winga wa kimataifa wa Nigeria na Spartak Moscow Victor Moses, 31.

Everton watamuuza mshambuliaji wa kimataifa wa England Dominic Calvert-Lewin, 25, ambapo Arsenal na West Ham United wanaonyesha matamanio ya kuinasa saini yake.

Kocha wa Ajax Erick ten Hag anashangazwa bado hajapewa mkataba wowote na Manchester United licha ya kuwaambia kuwa fedha haziwezi kuwa kikwazo cha yeye kutua Old Trafford.

Author: Bruce Amani