Tetesi za Mastaa Ulaya: Barcelona yasaka saini ya Aubameyang, Martial atakiwa Atletico

224

Newcastle United wamefanya mazungumzo ya awali ya Dele Alli, 25, wa Tottenham Hotspur kwa ajili ya kumsajili katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.

Huenda kiungo mshambuliaji wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba 28, akaondoka mwishoni mwa msimu huu baada ya kandarasi yake kumalizika klabuni hapo.

Atletico Madrid wanajaribu kumshawishi mshambuliaji wa Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 26, kuona kama anaweza kukubali kujiunga na timu hiyo.

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ameonyesha kutoluwa na shida na Real Madrid ambayo inahitaji huduma ya beki wa kati Antonio Rudiger, 28, hata hivyo yeye anahitaji kumrejesha Eden Hazard, 30, katika viunga vya Stamford Bridge.

Barcelona wanaendelea kuangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Gabon na Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, 32, ambaye amekuwa na wakati mgumu The Gunners pamoja na kuvuliwa kitambaa cha unahodha.

Author: Bruce Amani