Uganda Yaichapa Tanzania Kwa Mkapa Kufuzu AFCON 2023

223

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imefungwa bao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Uganda katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON nchini Ivory Coast.

Matokeo hayo ya ushindi yanaisogeza Uganda mpaka alama nne katika nafasi ya tatu wakati Tanzania ikisalia nafasi ya pili kwa alama sawa na Uganda baada ya michezo minne.

Bao kwenye mechi hiyo limefungwa dakika za lala salama na Rogers Mato Kassim ambaye alimzidi kipa Aisha Manula kwa mpira kuingia kambani.

Michezo ijayo itakuwa mwezi Juni kati ya Niger na Tanzania na Uganda dhidi ya Algeria kabla ya mechi za marudiano.

Author: Asifiwe Mbembela