Watu watatu ndani ya timu ya Cologne inayoshiriki Bundesliga wapata Corona katika kipindi hiki ambacho timu inaendelea na mazoezi

46

Watu watatu ndani ya klabu ya Cologne inayoshiriki ligi kuu ya Bundesliga nchini Ujerumani wamekuwa na maambukizi ya virusi vya Corona ingawa viongozi wa timu hiyo wamesisitiza kuwa mazoezi yataendelea kama ilivyopangwa.

Ligi ya Ujerumani ambayo huenda ikawa ligi ya kwanza barani Ulaya kurejea kwenye ushindani kama kawaida baada ya kuwepo kwa fununu kuwa serikali imetoa kibali cha Mei 16 au 23 inategemea na hali yenyewe.

Awali kulikuwa na maelekezo kuwa Bundesliga ingerudi Mei 9 lakini serikali nchini humo iliendelea kuweka vikwazo zaidi juu ya mikusanyiko.

“Wote waliopimwa na kukutwa na dalili za COVID-19 watabakia karantini kwa siku 14 kwa ajili ya uangalizi maalumu” ilisema taarifa ya klabu.

“Timu nzima, kuanzia waalimu, viongozi wa timu na hata wachezaji walifanyiwa vipimo siku ya Alhamis lakini katika majibu yaliyotoka ni kuwa wenzetu watatu wako na COVID-19”.

Wakati hayo yakijiri ndani ya FC Koln imesema wanafimilia wa timu hiyi watakaobainika kuwa na dalili au ugonjwa wenyewe hawatajwa majina kwani ni faragha yao. Mazoezi yataendelea kama kawaida huku tukichukua tahadhari zote za wataalamu wa afya.

Bundesliga iliwataka wachezaji kurejea mazoezi tangu Aprili 6.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani siku ya Alhamis alisema maamuzi ya ni lini shughuli za kimichezo zitaruhusiwa kuendelea nchini humo itajulikana Jumatano ya Mei 6.

Ligi kuu Ujerumani na ligi zote rasmi zilisimamishwa tangu katikati ya mwezi wa tatu hadi sasa haitaendelea ambapo siku za usoni kumekuwa na matumaini ya kurejea kwa ligi hiyo.

“Ni muhimu sana kujikita katika kuchukua tahadhari zote za wataalamu wa afya katika kipindi hiki,” alisema Merkel.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Ujerumani lilitoa tahadhari kuwa hasara kubwa itatokea endapo ligi haitaendelea kufikia mwezi Juni.

Mechi tisa zimesalia ligi kumalizika, Cologne wanakamata nafasi ya 10 kwenye msimamo wa Bundesliga.

Author: Bruce Amani