Gor na Kariobangi Sharks zapenya katika michuano ya CAF

64

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya kandanda nchini Kenya, KPL Gor Mahia wamefuzu katika hatua ya mchujo ya michuano ya Kombe la ligi ya mabingwa barani Afrika.

Kogallo wamepiga hatua baada ya kuifunga Nyasa Big Bullets ya Malawi magoli 4-3 kupitia kwa matuta ya penaliti. Mechi hiyo iliamuliwa kwa njia ya penaliti baada ya Nyasa Big Bullets kuifunga Gor Mahia goli 1-0 katika mkondo wa pili ushindi sawa na wa Gor Mahia katika mechi ya mkondo wa kwanza.

Mechi ya mkondo wa kwanza ilishia kwa ushindi wa goli 1-0 kwa faida ya Gor Mahia.

Wakati huo huo wawakilishi wa Kenya katika michuano ya Mashirikisho ya mabara Kariobangi Sharks wamefuzu katika hatua ya muondoano kabla ya kutinga hatua ya makundi.

Sharks imejikatia tiketi ya awamu ya pili baada ya kuifunga Arta Solar ya Djibouti mabao 3-0 ugenini. Kufuatia ushindi huo sasa Kariobangi Sharks itakutana na Asante Kotoko ya Ghana katika hatua ya mchujo.

Author: Bruce Amani