Wazito FC Wamtimua Kocha Kimanzi

195

Klabu ya Wazito FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Kandanda Kenya FKFPL imefikia mwafaka wa kumtimua kwenye timu hiyo kocha mkuu Francis Kimanzi pamoja na jopo nzima la makocha kufuatia mwendelezo wa matokeo mabaya.

Kipindi anateuliwa Kimanzi ambaye ni kocha wa zamani wa Mathare United kulikuwa na matumaini kibao kwamba huenda Wazito itafufuka lakini ndiyo kwanza anaondoka ikiwa kwenye mstari wa kushuka daraja katika nafasi ya 16 alama tisa katika mechi 13.

Wazito ikiwa chini ya Kimanzi ilianza kwa kuchezea kichapo kutoka kwa Kariobangi Sharks ambapo ilifungwa goli nne hali kadhalika amefutwa kazi baada ya kukiongoza kikosi hicho kufungwa bao nne dhidi ya Vihiga Bullets.

Akiwa na wastani wa kupoteza mechi kwa asilimia 42 na kushinda asilimia 31, Kimanzi ameiongoza Wazito katika mechi 45 ambapo ameshinda mechi 14, akishinda mechi 14 sare 12 na kufungwa michezo 19.

Author: Bruce Amani