Yanga yaishushia zigo la goli Ihefu Kombe la ASFC

486

Wanafainali wa Kombe la Shirikisho la TFF, klabu ya Yanga wameanza vyema kampeni ya kuwania taji hilo kwa msimu huu 2021/22 baada ya kuitandika Ihefu FC bao 4-0 katika mchezo uliopigwa dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Disemba 15.

Ushindi wa Yanga leo ambao umechagizwa na ubora wa mshambuliaji wa kati wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Heritier Makambo ambaye ameingia kambani mara tatu (hat-trick) huku bao lingine likiwekwa kimiani na Khalid Aucho.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga ambayo msimu uliopita walifika fainali na kupoteza kwa Simba bao 1-0, wanatinga raundi ya nne bora ya ASFC.

Magoli ya Makambo bila shaka yanaweza kuamsha hali ya upambanaji zaidi kwake kwa lengo la kumshawishi Mwalimu Nasreddine Nabi Mohamed kuanza kumpa dakika zaidi kwenye timu ya kikosi cha kwanza baada ya Fiston Mayele.

Author: Asifiwe Mbembela