Bila Lwandamina hakuna tatizo Azam, yaipiga Warriors

131

Kikosi cha Azam Fc kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Greeen Warriors katika mchezo wa Kombe la Azam Sports Federation Cup( ASFC) mtanange uliopigwa dimba la Azam Complex nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Ushindi huo unaifanya Azam kuungana na timu kama Mtibwa Sugar, Geita Gold, Yanga na Simba kutinga raundi ya Nne Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo dakika ya nne katika mchezo wa kwanza baada ya kufukuzwa kocha Mzambia, George Lwandamina, akimpa mwanzo mzuri kocha anayekaimu, Mmarekani mzaliwa wa Somalia, Abdihamid Moalin.

Author: Asifiwe Mbembela