Arsenal yakwea “Top Four” yaipiga West Ham United

183

Arsenal imekwea mpaka nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England hii ni baada ya kushinda goli 2-0 dhidi ya West Ham United mtanange uliopigwa dimba la Emirates Disemba 15.

Arsenal ikicheza mchezo wa pili bila ya kuwepo kwa aliyekuwa nahodha wa timu hiyo raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang wameonekana kutokosa kitu ambapo bao la kwanza lilipatikana kupitia kwa Gabriel Martinell wakati goli la pili likiwekwa kambani na Emile Smith Rowe kufunga hesabu za ushindi kwa kocha Mikel Arteta.

Wagonga Nyundo wa Jiji la London West Ham United walilazimika kumaliza mtanange huo pungufu kufuatia Vladimir Coufal kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi.

Alexander Lacazette alikosa penati na nafasi mbalimbali The Gunners walipoteza ambazo zingewapa ushindi mkubwa baada ya kupitia wakati mgumu.

Author: Bruce Amani