Yanga yatua Morocco, yaungana na kocha wao Nassredine Nabi

332

Yanga imewasili Jijini Casablanca Morocco tayari kwa maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na michuano mingine kama Ligi ya Mabingwa Afrika 2021/22.

Yanga imewasili ikiwa na kundi la wachezaji 21 waliotokea jijini Dar es Salaam kupitia Dubai huku wengine wakitangulia na mmoja atafuata nyuma.
Wakati kundi hili likifika tayari wachezaji watatu walishawasili ambao ni kipa Diarra Djigui, beki mpya Yannick Bangala ambaye bado hajatambulishwa rasmi na mshambuliaji Yacouba Sogne huku kiungo Khalid Aucho akitarajiwa kuwasili kesho Jumanne Agosti 17.
Tayari pia makocha wao ukianzia kocha mkuu Nesreddine Nabi na wasaidizi wake wawili pia walishatangulia kufika.
Mara baada ya kuwasili Yanga ilipokelewa na wenyeji wao ambao ni maafisa wa klabu ya RS Berkane. Yanga itakuwa hapa kwa kambi ya simu zisizopungua 10 wakijiandaa na maandalizi ya msimu mpya

Author: Asifiwe Mbembela