Zidane akana taarifa za kufutwa kazi Real Madrid

95

Kocha Mkuu wa klabu ya Real Madrid inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania Zinedine Zidane amesisitiza kuwa hayupo kwenye presha ya kuondolewa klabuni hapo baada ya matokeo ya aibu dhidi ya Shakhtar Donetsk mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopigwa katikati ya wiki iliyopita.

Ikiwa nyumbani, Madrid ilikubali kichapo cha goli 3-2 dhidi ya Shakhtar lakini maneno ya Zidane kuelekea mtanange wa El Classico siku ya Jumamosi dhidi ya Barcelona yanadai ana uhudiano mzuri na Rais wa timu hiyo Florentino Perez.

Madrid na kocha wake watasafiri kwenda dimba la Camp Nou dhidi ya Barcelona baada ya matokeo hasi katika mechi mbili mfululizo, moja dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu ya Cadiz kwenye mbio za La Liga na ya Uefa.

“Sina hofu, kila mmoja anajua hilo, nawaamini wachezaji na wachezaji wananiamini mana tumeshinda pamoja hapa mataji na mechi nyingi, sina hofu kabisa” alisema Zidane. “Tunauwezo wa kuwashangaza watu kwenye mechi yetu ya kesho”. Amesema Zizou.

Author: Bruce Amani