Arteta asema hahofii kufutwa kazi Arsenal baada ya mwanzo mbaya katika ligi

183

Kocha Mkuu wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta amesema hana hofu ya kufutwa kazi katika nafasi yake hiyo baada ya rekodi ya matokeo mabaya mwanzoni mwa msimu huu ambayo ilikuwa haijavunjwa tangu mwaka 1981. Arsenal walipata kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Wolverhampton Wanderes katika mchezo uliomalizika kwa maumivu kutokana na mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez kupata majeruhi ya kichwa.

Arsenal ambayo ilianza vyema kwenye mechi za awali inakamata nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini England baada ya kushindwa mechi 5 kati ya 10, ikiwa ni mwaka mmoja tangu Unai Emery kufutwa kazi Emirates.

“Ni kitu ambacho nilikijua tangu nimechagua kuwa kocha kuwa kuna siku nipata nafasi ya kuwa kocha, na siku nyingine nitafukuzwa kazi, lakini hapa sijui kinachoendelea”. Alisema

“Katika taaluma hii najua kuna siku itatokea, hivyo sihofii chochote”.

Magoli ya wageni Wolves yalifungwa na Neto kwenye dakika ya 22 na dakika ya 42 bao lililofungwa na Daniel Podence akitumia vyema makosa ya walinzi wa Arsenal na mlinda mlango Bernd Leno.

Gabriel aliwapatia goli la kufuatia machozi wenyeji wa mchezo huo likiwa bao lake la kwanza ndani ya uzi wa Arsenal mlinzi huyo akimalizia mpira wa winga wa zamani wa Chelsea Willian. Wolves, wanakamata nafasi ya sita wakiwa alama nne pungufu kuelekea nafasi nzuri zaizi kwenye msimamo wa EPL.

Author: Bruce Amani