Chama aaga mashabiki Simba

492

Clatous Chota Chama amewaaga rasmi mashabiki pamoja na viongozi wa Simba baada ya nyota huyo kutimikia katika timu ya RS Berkane ya nchini Morocco kwa usajili unaotajwa kuwa wa gharama kubwa.

Chama ametumia ukurasa wake wa Twitter kuandika kuwa “Nimekuwa kimya kwa muda tangu mara ya mwisho nitume ujumbe wowote kwenye kurasa zangu za kijamii, ilibidi iwe hivyo kwa sababu kuna mambo nilikuwa ninakamilisha na nilikuwa nasubiri taratibu zote zikamilike, siwezi kuwaacha nyinyi kwenye giza,”

“Siwezi kueleza namna ninavyohisi kuhusu Simba, kwa maneno machache ni kwamba bado ni ngumu kuamini kwamba jina langu halitatajwa na Baraka Mpenja msimu ujao ama sitavaa jezi yangu namba 17, katika timu ambayo ilikuwa ni ya nyumbani,”

Katika hatua nyingine, Chama amemshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohamed Dewji MO, Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez na viongozi wengine na mashabiki wa klabu ya Simba.

“Kwa mashabiki nitazidi kuwakumbuka nasema asante sana nitazidi kuwasiliana nanyi kupitia mitandao ya kijamii, nitaendelea kushangilia pamoja nanyi labda ikitokea nikacheza nanyi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa heri na

Author: Asifiwe Mbembela