Chelsea yashinda kwa Brentford na kurejea usukani mwa ligi

288

Chelsea imerudi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini England hii ni baada ya kuibuka na ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Brentford katika mchezo wa dabi ya London uliopigwa Leo Jumamosi Octoba 16 huku bao la Ben Chilwell likiamua matokeo.

Baada ya ushindi mzito wa Liverpool kwa Watford walikwea kileleni lakini kikosi cha kocha Thomas Tuchel kiliwanyamazisha Brentford na kurudi juu ya msimamo wa EPL ikiwa ni baada ya masaa machache.

Beki huyo wa kushoto wa England alifunga goli kunako dakika ya mwisho kabisa ungwe ya kwanza, likiwa ni bao la tatu katika mechi tatu za klabu na timu.

“Kuna dakika walicheza vizuri (Brentford) kuliko sisi kwa sababu sisi tulikubali kurudi nyuma na kutengeneza safu ya kujilinda kuhakikisha hatupoteza alama”, alisema Tuchel.

Author: Bruce Amani