Martial ataka kuondoka Man United

280

Wakala wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa na Manchester United Anthony Martial amesema mchezaji huyo anahitaji kuondoka Old Trafford.

Martial mwenye umri wa miaka 26, ameanza mechi mbili pekee kwenye Ligi msimu huu na kufunga bao moja, na hajacheza mechi yoyote chini ya kocha mpya Ralf Rangnick.

“Anthony anapendelea kuihama klabu hiyo”, alisema Wakala wake Philippe Lamboley.

“Anahitaji sehemu ambayo atapata nafasi ya kucheza, haitaji kubakia Januari, nitaongea na Manchester hivi karibuni kujua hatima yake”.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo wa wikiendi hii dhidi ya Norwich City, Ralf Rangnick kocha wa Man United amesema “kama mchezaji atakuwa hapati nafasi ya kucheza haina maana kuendelea kuwa naye ni kheri akaondoka hata kwa mkopo”.

Author: Asifiwe Mbembela