Michango ya Wanasimba Yaridhisha – Try Again

191

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salum Abdallah ‘Try Again” amesema zoezi la wanachama kuchangia fedha za ujenzi wa Uwanja wa klabu hiyo linaendelea vizuri.

Akizungumza Leo Jumanne Jijini Dar es Salaam, Abdallah maarufu kama “Try Again” amesema ndani ya muda mfupi tangu kuzinduliwa kwa zoezi hilo Desemba 17, idadi kubwa ya wanachama imechangia fedha, jambo ambalo linatia moyo kuendelea kuhamasisha.

Mpango huu ni wazo la Mwanahisa Mkuu Simba, Mohamed ‘Mo’ Dewji ambaye ameahidi kutoa Sh. Bilioni 2 ili wanachama wajazie klabu hiyo ijenge Uwanja wake kuepuka adha inazokutana nao kutumia Uwanja usio wake.

Kwa sasa Simba ina Uwanja wa mazoezi tu, Mo Simba Arena uliopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na mechi zake za mashindano inatumia Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Bajeti ambayo imetajwa kuwa inaweza kukamilisha ujenzi wa uwanja huo bilioni 30.

Author: Bruce Amani