Mtibwa Sugar yatibua furaha ya Simba kwa kuikaba sare ya 1 – 1

328

Raundi ya pili ya Ligi Kuu nchini Tanzania imeendelea kwa michezo kadhaa katika viwanja tofauti tofauti ambapo mtanange uliotupiwa macho ni ule uliopigwa dimba la Jamhuri Mjini Morogoro ambapo Mtibwa Sugar waliikaribisha Simba SC.

Katika mechi hiyo, mabingwa watetezi wamebanwa mbavu kwa kutoa sare ya goli 1-1 na kufikisha pointi nne kwa upande wa Simba wakati klabu ya Mtibwa Sugar ambayo inanolewa na zao la Turiani Zuberi Katwila inafikisha pointi 2.
Goli la Simba limefungwa na kiungo mkabaji Mzamiru Yasni ambalo lilikuwa bao lake la pili katika michezo miwili ya mwanzo awali alitupia katika mtanange uliopigwa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya dhidi ya Ihefu.
Wakati bao la Mtibwa Sugar limewekwa kimiani na Boban Zirinstuta akimalizia mpira wa kutengwa wa Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ ungwe ya pili ya mchezo huo.
Baada ya mtanange huo, Simba watarudi Dar es Salaam kumenyana na Biashara United ukiwa ni mwendelezo wa VPL Sugar watakuwa na kibarua kizito kuwakabili Ihefu dimba la Sokoine Mbeya.
KWINGINEKO.
Mechi ya pili mfululizo kwa Dodoma kupata matokeo chanya katika mechi mbili za nyumbani (JKT Tanzania 0-2 Dodoma Mji Fc).
KMC wameshinda mechi zote mbili za nyuma za VPL wakati Tanzania Prisons wakisare ya kwanza na kupoteza hii ya pili sasa wanarejea Rukwa, Sumbawanga dimba la Nelson Mandela(KMC 2-1 Tanzania Prisons).

Author: Asifiwe Mbembela