Tanzania yaibamiza Burundi yatwaa ubingwa Cecafa U-23

271

Timu ya Taifa ya Tanzania ya chini ya umri wa miaka 23 imetwaa ubingwa wa mashindano ya Cecafa U-23 baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati Burundi katika mchezo wa fainali uliopigwa dimba la Bahir Dar Ethiopia Leo Ijumaa Julai 30.

Ushindi wa Tanzania umepatikana kwa penalti 6-5 dhidi ya Burundi baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare tasa kisha mikwaju ya penati ikachukua nafasi yake.

Tanzania inayonolewa na kocha Kim Poulsen ilipata nafasi ya kubeba taji hilo mbele ya Rais wa Shirikisho la Kandanda Tanzania Wallace Karia baada ya penalti ya mwisho ya kijana Rajab Athuman kuingia nyavuni wakati ambao tuta la mchezaji wa Burundi Akizamana kugonga mtambaa wa panya

Poulsen amesema:”Ni furaha kwangu na vijana pamoja na taifa kiujumla kwa kupata matokeo mazuri ambayo tulikuwa tunahitaji.

“Ilibidi nifanye mabadiliko kwenye kikosi kwa sababu wachezaji walikuwa wamechoka kutokana na kucheza mechi nyingi za ushindani ila mwisho wa siku tmeshinda,” .

Rais wa TFF Wallace Karia amesema kuwa ni jambo la furaha kwa Tanzania kuweza kutwaa ubingwa huo hivyo bado kazi inaendelea

Alikuwepo pia makamu wa Kwanza wa Rais Athuman Nyamlani nchini Ethiopia ambapo walishuhidia Tanzania ikitwaa taji la Cecafa.

Author: Asifiwe Mbembela