Trent Alexander-Arnold aongeza kandarasi Liverpool

267

Beki wa mpira wa Liverpool Trent Alexander-Arnold ameongeza mkataba wa kuendelea kusalia ndani ya Liverpool mpaka kiangazi cha mwaka 2025.

Alexander-Arnold, 22, akiwa zao la Liverpool amecheza jumla ya mechi 179 tangia kucheza mechi yake ya kwanza Octoba 2016.

Alexander-Arnold, ambaye ndani ya kipindi hicho ameisaidia Liverpool kushinda taji la Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 pamoja na ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Kuongeza mkataba wa kubakia hapa siku zote ni jambo njema kwangu, familia yangu. Nimekuzwa mazingira haya(Anfield) ni klabu inayonijua vyema tangia utoto”.

Alexander-Arnold alitajwa kama wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora duniani Ballon d’Or mwaka 2019 baada ya kushinda Kombe la Dunia ngazi ya klabu naa Uefa Super Cup.

 

Author: Asifiwe Mbembela