Manchester City yatuma Ofa nzito kwa Aston Villa kumnasa Grealish

109

Manchester City imetuma rasmi ofa ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa England na Aston Villa Jack Grealish ya pauni milioni 100.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameweka jina la kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 kama chaguo la kwanza kwenye dirisha kubwa la usajili la kiangazi msimu huu.

Inaeleweka kuwa klabu hizo mbili zilikuwa kwenye mawasiliano ya karibu tangia msimu unaanza.

City wanajaribu kuharakisha kukamilika kwa uhamisho wa mchezaji huyo kabla hajarejea kwenye kikosi cha Villa kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao 2021/22.

Author: Bruce Amani