Arsenal yakamilisha usajili wa Ben White kutokea Brighton

349

Arsenal imekamilisha uhamisho wa beki wa kati wa Brighton Ben White kwa dau la pauni milioni 50 baada ya mazungumzo ya muda mrefu.

Mlinzi huyo wa miaka 23, alikuwa sehemu ya kikosi cha England ambacho kilifika fainali ya Euro 2020 na kupoteza kwa Italia amekubali kandarasi ya muda mrefu kuwepo dimba la Emirates.

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta akimzungumzia mchezaji huyo amesema “Ben White ni mchezaji mzuri, alikuwa hitaji letu, ni hatua nzuri kukamilisha uhamisho kabla ya msimu kuanza”

Ben White amepita klabu ya Southamption ambayo nchini England imekuwa ikitajwa kama sehemu ya kukuzia wachezaji kutokana na wachezaji wengi wanaong’aa katika klabu kubwa kutokea viunga hivyo kabla ya kujiunga na Brighton mwaka 2016.

Unakuwa usajili wa tatu kwa The Gunners baada ya kiungo Albert Sambi Lokonga kutokea Anderlecht na beki wa kushoto Nuno Tavares kutokea Benfica.

White atakuwa anavalia jezi namba nne ambayo ilikuwa inavaliwa na beki wa Kibrazil David Luiz aliyeondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu uliopita.

Author: Asifiwe Mbembela