Aguero afanya mazungumzo na Barcelona ili kujiunga nao mwishoni mwa msimu

175

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Sergio Kun Aguero amefanya mazungumzo na klabu ya Barcelona kwa minajili ya kujiunga na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Aguero, 32, ataondoka klabuni Man City baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu akiwa amecheza mechi 388 na kufunga goli 258.
Barcelona wanahitaji huduma ya mshambuliaji huyo kutokana na hali mbaya ya uchumi ndani ya klabu, uliochagizwa na janga la virusi vya Corona.
“Dili bado halijakamilika lakini pande zote mbili zimekutana na kuzungumza juu ya hatima yao” alisema mwandishi mkongwe wa nchini Hispania Guielleme Balague.
Aguero ni rafiki mkubwa wa Lionel Messi na inatajwa kuwa moja wapo ya sababu ya kumchukua mchezaji huyo wote wakiwa wenyeji wa Argentina.
Hata hivyo, Barcelona bado imekuwa ikuhusishwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa England Harry Kane, na wa Norwei Erling Braut Haaland.

Author: Bruce Amani