Tetesi za Mastaa Majuu: Pjanic kujiunga na Barcelona mwishoni mwa msimu, Sancho awekewa ngumu kutoka Dortmund

236

Manchester United hawatalipa zaidi ya pauni milioni 50 kwa ajili ya winga wa Borrusia Dortmund na England, lakini wenye mchezaji Dortmund wanasema mchezaji wao haondoki bila kuwepo kwa pauni milioni 100.

Arsenal wanafikiria kumuachia kiungo mkabaji wa timu hiyo Matteo Guendouzi, 21, kwenda Atletico Madrid kwa ajili ya kumnasa kiungo mkabaji mwingine wa Thomas Partey, 27.

Manchester City wameanza kuwania saini ya beki wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 25, ingawa watakutana na changamoto kubwa kutoka kwa Chelsea ambao wanataka kumrudiasha tena.

Kiungo mkabaji wa Juventus Miralem Pjanic, 30, atajiunga na timu ya La Liga Fc Barcelona mwishoni wa msimu huu.

Beki wa kulia wa Real Madrid na Morocco Achraf Hakimi, 21, ametua rasmi nchini Italia kwa ajili ya kukamilisha dili la kusaini katika klabu ya Inter Milan kwa dau linalokadiliwa kufikia pauni milioni 36.

Mshambuliaji wa Arsenal ambaye anakipiga kunako klabu ya Roma ya Italia Henrikh Mkhitaryan ameongezewa mkataba maalumu wa kumalizia msimu huu katika klabu hiyo, raia huyo wa Armenia alijiunga na Roma mwezi Septemba.

Author: Bruce Amani