Manchester United wachangamsha mbio za Ulaya kwa kuwabugiza Brighton Hove Albion

358

Manchester United imepata ushindi wa 15 mfululizo wa ligi baada ya kuichabanga Brighton Hove Albion goli 3-0 na kuwa karibu kuingia nafasi za tiketi za kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kikosi cha Kocha Ole Gunnar Solskjaer kilitawala dimba la Amex kwa kiasi kikubwa ambapo ushindi huo umeifanya ipande alama mbili chini ya Chelsea.

Kinda Mason Greenwood alianza kwa kuwatanguliza kwa shuti dogo ndani ya kumi na nane akimpita mlinzi Lewis Dunk akimalizia pasi ya Aaron Wanna Bisaka.

Ingizo jipya la mwezi Januari Bruno Fernandes aliandikisha goli la pili la mchezo kwa kutumia pasi ya kiungo mweza Paul Pogba mpira ambao uliguswa na kumpoteza mabawa mlinda mlango wa timu hiyo.

Goli la mwisho liliwekwa kimiani na kiungo huyo akiifungia goli la shambulizi la haraka ama (counter-attack) baada ya mpira wa Mason Greenwood.

Author: Bruce Amani