Barcelona yaanza kibabe mbio za La Liga yaichapa 4 – 0 Villarreal

493

Kocha wa Barcelona Ronald Koeman amepata ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Villarreal katika mchezo wake wa kwanza ndani ya La Liga huku nahodha wa kikosi hicho Lionel Messi akifunga bao moja katika ushindi huo mnono.

Kinda wa kikosi hicho Ansu Fati alikuwa mchezaji muhimu wa mechi baada ya kufunga goli mbili katika mechi hiyo, bao la kwanza akimalizia pasi ya Jordi Alba na bao la pili akitumia vyema mpira wa Philippe Coutinho.

Hata hivyo kinda huyo alihusika katika bao la tatu kwani ndiye aliye sababisha penati ambayo alipigwa na kepteni Messi na kufanya matokeo kuwa 3-0 kabla ya Pau Torres kujifunga akishindwa kuokoa vizuri krosi ya Messi.

Akiwa katika majukumu mapya kwa maana ya klabu, kocha Unai Emery wa Villarreal alishindwa kuonyesha upinzani kwani alihitaji dakika za lala salama kuandikisha shuti lililolenga lango.

Messi anakuwa mchezaji wa 60 kufunga bao kwenye misimu 17 tofauti ya La Liga, mchezaji mwingine ni Sergio Ramos ambaye rekodi hiyo ameifikia siku ya Jumamosi.

Author: Asifiwe Mbembela