Beki wa Man United Harry Maguire kuendelea kukaa nje

392

Mlinzi wa Manchester United Harry Maguire huenda siku za kukaa nje ya dimba zikaongezeka baada ya kuukosa mchezo wa Manchester dabi sasa huenda akaendelea kuwa mtazamaji kwa kipindi kirefu kutokana majeruhi.

Hakuna namba rasmi ya mechi atakazo kosa licha ya kocha Ole Gunnar juzi Jumanne kuthibitisha kuwa hata chelewa kurudi uwanjani kwa sababu ana maumivu madogo ya kifundo cha mguu.

Maguire alipata majeraha hayo kwenye mchezo wa wikendi iliyopita dhidi ya Wolves mtanange wa FA hatua ya tatu uliomalizika kwa sare ya tasa.

Hivi sasa Harry Maguire ambaye ni mlinzi wa England anategemewa kukosa mechi ya marejeano wa nusu fainali ya Carabao dhidi ya Manchester City, mechi mbili ya ligi kuu na ule mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya Wolves..

Klabu ya Man United tayari ina changamoto ya majeruhi kwenye eneo la ulinzi kwani Axel Tuanzebe na Eric Bailly wote wapo nje, huku Chris Smalling akiwa Roma kwa mkopo.

Author: Bruce Amani