Chelsea yachomoka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Leeds United

153

Chelsea imeibuka kidedea mbele ya Leeds United kwa kufunga goli 3-2 huku shujaa akiwa ni Antonio Rudiger ambaye alisababisha matuta mawili yote yakifungwa na kiungo mkabaji Jorginho.

Pengine ni bahati baada ya awali kutanguliwa Chelsea kwa bao la Raphinha ambaye alifunga goli kwa penati ungwe ya kwanza kabla ya Chelsea kusawazisha kupitia kwa kiungo Mason Mount akimalizia pasi ya Marco Alonso.

The Blues walitangulia kupata goli pili kupitia kwa Jorginho aliyefunga kwa penati kufuatia Rudiger kufanyiwa madhambi kabla ya Leeds United ya Marcel Bielsa kusawazisha bao hilo akilifunga Joe Gelhardt.

Jioni Jorginho alifunga goli la tatu na la ushindi kwa Chelsea ambayo imeirudisha Chelsea kwenye mbio za ubingwa ambapo sasa wanakuwa nyuma alama mbili kwa Manchester City ambao wameshinda bao 1-0 dhidi ya Wolves na Liverpool kushinda bao 1-0 dhidi ya Aston Villa.

Author: Bruce Amani