Chelsea Yaibuka Kidedea Mbele ya Crystal Palace EPL

120

Chelsea imevuna alama tatu muhimu mbele ya Crystal Palace baada ya kushinda kwa goli 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa dimba la Selhurst Park Leo Jumamosi Februari 19.

Ushindi wa Chelsea ambayo ilikuwa haijacheza mechi yoyote tangia kushinda dhidi ya Tottenham mwezi mmoja uliopita, umekuja wakiwa pia wamepumzika takribani wiki moja tangia kushinda taji la Kombe la Dunia ngazi ya klabu Jumamosi iliyopita.

Ulionekana kama mchezo ambao unaenda kumalizika kwa sare tasa baada ya timu zote kuwa na kosa kosa za hapa na pale, mpaka pale ambapo winga wa kimataifa wa Morocco Hakim Ziyech kufunga goli dakika za mwishoni ungwe ya pili.

Kwa matokeo hayo, kocha Thomas Tuchel atakuwa anaona nafasi ya kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao yanabakia hai baada ya kiwango cha timu hiyo kuwa kwenye wakati mgumu nyakati fulani.

Author: Bruce Amani